Hili linajulikana na huonysha tatizo; haimaanishi kwamba Google huiona Tor kama ni spyware.
Utakapo iona Tor yako, unatuma maswali kupita exit relay ambazo zimesambazwa na maelefu ya watumiaji wengine. Watumiaji wa Tor wanaona ujumbe huu pale watumiaji wengi wa Tor wanapouliza Google kwa muda mfupi. Google hukatiza kiwango cha juu cha traffic katika anwani ya IP moja (exit relay uliyoichagua) kama mtu anayejaribu kufuatiza tovuti, hizo inapunguza traffick kutoka kwenye anwani ya IP kwa muda mfupi.
Unaweza kujaribu Circuit mpya kwa tovuti hii kuzipata tovuti kutoka kwenye anwani za IP tofauti.
Maelezo mbadala ni kwamba Google hujaribu kugundua aina fulani za spyware au virus ambazo hutuma maswali tofauti katika ukurasa wa kutafuta wa Google. Inakumbuka anwani za IP kutoka kwenye maswali yote yaliyopokelewa (hawajagundua kuwa ni exit relay za Tor), na wanajaribu kutoa angalizo kwa mawasiliano yoyote yanayotoka kwenye anwani za IP ambazo maswali ya hivi karibuni huonyesha tatizo.
Kwa uwezo wetu, Google haifanyi kitu chochote kwa kukusudia hususani kuzuia au kudhibiti matumizi ya Tor. Ujumbe wa dosari kuhusu mashine iliyoathirika itafutika baada ya muda mfupi.